Alhamisi , 17th Sep , 2020

Baadhi ya wauzaji wa baiskeli zilizotumika (used) jijini Dar es Salaam wamesema bei ya jumla kwa baiskeli hizo imepanda kutoka shilingi elfu 40 Hadi kufikia shilingi 80(elfu themanini) kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Covid 19.

Baadhi ya wauzaji wa baiskeli wakiziandaa kwaajili ya kuwauzia wateja

Waswahili wanasema linalowezekana leo lisingoje kesho msemo huu ukisemwa na moja ya wauzaji wa baiskeli hizo ambaye ameoneshwa kuumizwa na hali ya biashara hiyo ilivyo kwa sasa kwa kuwa mataifa mengi ambayo huzifuata bidhaa hizo mengi bado yanalia na janga la Covid 19.

"Kipindi cha nyuma ulikuwa unashusha kontena haraka tuu mzigo unachukuliwa lakini saizi hapa nyuma kidogo unapesa lakini huwezi kwenda nje kufata mzigo ndo maana moja kwa moja baiskeli zimepanda bei tofauti na ilivyokuwa "-Hamis Bones muuzaji wa baiskeli

Bw Hamisi amesema biashara hiyo imeajiri watu wengi wakiwemo mafundi ambao huzirekebisha mara baada ya mzigo kufika, vijana waoshaji huku wao wenyewe wakielezea namna biashara hiyo inavyochangia katika maisha yao ya kila siku.

"Yani kiukweli kabla ya hali ya maradhi ya Covid 19 mzigo ulikuwa unatoka sana na kiukweli kipato kilikuwa kizuri tofauti na sasa zaidi tunaganga tuu ivyo ivyo"alisema mmoja ya Mafundi baiskeli Pius Adolfu.

Aidha wametoa wito kwa vijana bado muda wote wamekuwa wakilalamika juu ya ukosefu wa ajira kuthubutu kufanya lolote Ili kuondokana na adha hiyo.
Huku wakiiomba serikali kutichoka kuweka mazingira rafiki kibiashara.