Jumatano , 29th Mar , 2023

Wafanyabiashara katika soko la Mgandini na Ngamiani jijini Tanga wamepinga kuhusishwa na tuhuma za upandishwaji wa bei za bidhaa na badala yake wamesema bidhaa zilipanda hata kabla ya mwezi wa ramadhani kutokana na hali ya ukame ambayo ilisababisha kupatikana kwa mazao duni kwa wakulima.

Wafanyabiashara hao wametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman baada ya kutembelea wafanyabiashara hao na kufahamu hali halisi ya bei za bidhaa za vyakula katika masoko yaliyopo katika jiji la Tanga. 

Aidha, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga amesema ziara hiyo inalenga kusikiliza kero kutoka kwa wafanyabiashara na wateja wao na kuzitafutia ufumbuzi ikiwa ni agizo Mhe.Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan.