Jumatano , 6th Jul , 2022

Licha ya serikali kutoa ruzuku ya Sh bilioni 100 ili kupunguza bei ya mafuta nchini Tanzania wakati bei ya soko la dunia ilipopanda, bei za rejareja za mafuta nchini hapa zimepanda tena, ambapo Wilaya yenye gharama kubwa zaidi ya mafuta nchini Tanzania ni Kyerwa

Kyerwa inaongoza kwa bei kubwa ya mafuta

Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, inapakana na Rwanda na Uganda, ambapo lita moja ya petroli sasa inagharimu Sh3,458, dizeli Sh3,381 na mafuta ya taa Sh3,676 kwa lita. Mwezi Juni Kyerwa bei ilikuwa Sh3,539 kwa Petroli na Sh3,232 kwa dizeli.

Waendesha magari Jijini Dar es salaam wameanza kununua mafuta kwa bei mpya kuanzia leo Julai 6, 2022, lita moja ya petroli inanunuliwa kwa Sh3,220, wakati lita moja ya dizeli ikigharimu Sh 3,143 na bei ya rejareja kwa lita moja ya mafuta ya taa ikigharimu Sh3,442.

Bei hizo mpya zilitangazwa Jumanne, Julai 5, na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu kuanza kutumika kwa bei mpya baada ya ruzuku Juni 1, 2022 ambapo petroli ilishuka hadi 2,994 kutoka 3,301, diseli 3,131 kutoka 3,452 kabla ya ruzuku, wakati mafuta ya taa yalibakia 3, 299 kabala na baada ya luzuku ingawa kuanzia Julai 6, lita moja ya mafuta ya taa ni 3, 442 ikiwa ni ongezeko la Sh 143.