Jumatatu , 6th Jun , 2022

Kampuni ya Bia ya Serengeti imesema itaendelea kuchangia jitihada mbali mbali zenye lengo la kukuza sekta ya Kilimo na kuongeza tija kwa wakuima wa ndani.

Akiongea wakati wa kukabidhi vyeti kwa wanafunzi 27 wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, ambao wamepata udhamini wa masomo kupitia programu ya Kilimo Viwanda mkurugenzi wa mahusiano kwa umma wa kampuni hiyo John Wanyancha alisema SBL inatambua umuhimu wa Kilimo kwa uchumi na ipo tayari kuunga mkono jitihada za lkukikuza

"Lengo la udhamini huu ni kuona watanzania wanakuwa na uwezo wa kujitegemea kupitia kilimo na sisi tumeamua kulisimamia hili"alisema John Wanyancha, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Sinani Simba, alisema ufadhili wa SBL siyo tu umesaidia wanafunzi wanaosoma Kilimo na ambao wanataoka mwenye familia zenye kipato duni, bali pia kitasaidia kuongeza wataalamu katika sejta hiyo mama kwa uchumi.