Jumapili , 18th Oct , 2020

Serikali imesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita imefanikiwa kuruhusu mazao ya chakula, ikiwa ni pamoja na mahindi kuuzwa nje ya nchi, ambapo imesaidia kushuka kwa mfumuko wa bei kufikia asilimia 3.86 mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 5.59 mwaka 2015.

Bidhaa za vyakula zikiwa sokoni.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameyasema hayo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya chakula Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mji Mwema, mkoani Njombe.

Sekta ya kilimo imefanikiwa kuajili zaidi ya 65% ya nguvukazi na inachangia asilimia 30 ya pato la Taifa (GDP). Aidha, kilimo kinachangia takribani asilimia 65 ya malighafi za viwandani na asilimia 100 ya chakula kinachotumika nchini”, amesema Hasunga. 

Hasunga, amesema kuwa Wizara ya Kilimo katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imepata mafanikio makubwa ikiwamo kuchangia nchi kuingia mapema katika uchumi wa kipato cha kati mwaka 2019.