Jumatatu , 20th Jun , 2022

Ili kuyainua makundi maalumu ya machinga na vijana wa Bodaboda serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya Jamii imeingia makubaliano na Chama cha wahasibu TAA kufanya usimamizi na kutoa mafunzo kwa makundi haya ili kupitia wataalamu hao waweze kufahamu misingi ya kutunza fedha

Akitoa kauli hiyo mara baada ya kuingia makubaliano hayo kati ya Serikali, TAA na chama cha wamachinga SHIUMA amesema wamedhamiria kupata takwimu sahihi ili kuweza kuwaratibu wamachinga kote nchi nzima kujua walipo kwa mifumo hai iliyowekwa.

"Haiwezekani kuwa na watu ambao wao miaka nenda rudi hawakui kibiashara ndo maana sasa serikali imeangalia na kuweka sasa mifumo ambayo mmachinga atakuwa kibiashara" alisema Dr Mpanju ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii.

"Kama wahasibu wote nchi nzima watashirikiana basi taaluma yao itawasaidia wamachinga kujifunza kuweka bajeti ili kukuza mitaji yao" amesema CPA Victorius Kamuntu ambaye ni Makamu wa Rais TAA

Awali kabla ya makubaliano uongozi wa wamachinga taifa umeomba kwa serikali kuondoshwa kwa baadhi ya changamoto za kisera zilizopo kwa baadhi ya halmashauri nchini

Akisoma kwa wamachinga waiohudhuria makubailliano hayo mwanasheria wa Wizara  amesema ni muda sasa kwa wamachinga kutumia fursa hiyo kibiashara.