Jumatano , 9th Sep , 2020

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania bi Jacqueline Maleko amesema wanawake Wana uwezo wa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda na biashara endapo wataaminiwa na kupewa nafasi ya kufanya Hivyo.

Bi Jacqueline ametoa rai hiyo wakati akizindua tuzo za wanawake wafanyabiashara waliofanya vizuri kwa mwaka 2020 katika sekta za viwanda na biashara lengo ikiwa kutambua na kuthamini mchango wao sambamba na kujenga imani juu ya ujasiriamali pamoja na uwekezaji ambao wameufanya.

"Hili zoezi la washiriki wa tuzo litaendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja na litafungwa Tarehe 9 October 2020 huku sherehe za utoaji tuzo zikitarajiwa kufanyika Tarehe 28 Novemba 2020 hivyo niwaombe Sana msisite kujitokeza kwa wingi"

Aidha chama hicho kimeishukuru serikali kwa kuboresha mazingira ya  uwekezaji katika biashara na viwanda hali ambayo inaendelea kuongeza ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi. 

"Mchakato wa upatikanaji wa washindi wa tuzo unaratibiwa na kamati maalum inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi za Serikali na sekta binafsi, hii yote nikuwezesha wanawake wote wapate fursa na"alisema bi Maleko. 

Kwa upande wao wanawake wafanyabiashara nchini wesema jukwaa hilo limekuwa daraja la wao kukutana na watu wapya ikiwa ni pamoja na kutengeneza fursa mpya za kibiashara.

Utoaji wa tuzo hizo utaedana na uzinduzi wa jarida la wanawake 100 wajasiriamali waliothubutu litakalotumika kutangaza  kazi mbalimbali za wajasiriamali nchini ikiwa ni mkakati wa kuendeleza sera ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa viwanda.