Jumatano , 20th Sep , 2017

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu  amesema ameamua kuwashughukikia madereva wanaovunja sheria za barabarani kwani ni watu wanaojulikana.

Akizungumza kupitia kipindi cha East Africa Breakfast, Kamanda Musilimu amesema kuwa madereva wengi wamekuwa wakifanya makosa kwa mazoea kwa kuwa wamejua adhabu yao ni faini kwa makosa wanayofanya.

Kamanda Muslimu amesema, "Uzuri wangu mimi nadili na watu wanaojulikana, nawajua ni madereva ambao kila siku nawaona barabarani, Nitahakikisha wanatii sheria wenyewe bila kushurutishwa na watakaovunja sheria za barabarani wajue kuna maneno matatu tu - KA-MA-TA".

Pamoja na hayo hayo Kamanda Musilimu amesema propaganda za kwamba askari waliopo hawatoshi ni maneno ya watu tu lakini anaamini kuwa kikosi chake kina ngunu kazi ya kutosha.

'Watu ndiyo  wanasema askari wetu hawatoshi, Lakini kutokana na uchunguzi ambao tayari tumekwisha ufanya , kwa sasa tumejipanga kufanya doria katika maeneo hatarishi, ambapo huko sheria hazizingatiwi.  Huko barabarani si mnakutana nao basi mjue nina askari wanatosha," amesema

Ameongeza pia "Madereva wasijiulize sana faini wanazopigwa zinapokwenda kwa sababu wao wameshafanya makosa cha muhimu kwao ni kuwa makini ili waweze kuwa salama. Wengne wanasema kama tumekuwa tunakusanya mapato barabarani mimi nawaambia waache makosa waone kama watasumbuliwa".