Alhamisi , 27th Nov , 2014

Watu 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhi baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ''Thende Sheki'' kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo la Mkanyageni lililopo wilayani muheza.

Watu 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhi baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ''Thende Sheki'' kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo la Mkanyageni lililopo wilayani muheza.

Ajali hiyo ilikusanya mamia ya wananchi kutoka jijini Tanga, Muheza na Lushoto kwa ajili ya kwenda kushuhudia na kutambua miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa nje katika hospitali teule ya mtakatifu Augustino wilayani Muheza kwa ajili ya utambuzi ambapo hadi majira ya mchana miili ya watu 9 waliokufa papo hapo katika eneo la tukio ilitambuliwa na ndugu na jamaa.

Akielezea miili na majeruhi waliopokelewa katika hospitali hiyo, kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Muheza Dkt. Peter Shemkhai amesema watu wawili walifariki hospitali muda mchache baada ya kuletwa na kupatiwa tiba katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema dereva mwenye lori alikuwa akiyumba njia nzima kabla ya kukutana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Coaster hatua waliyodai kuwa ina viashiria vya dereva wa lori hilo alikuwa amepitiwa na usingizi wakati akiwa barabarani.

Kufuatia hatua hiyo madereva wa magari yote mawili ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza  kila mmoja alikuwa na haya ya kueleza kuhusu chanzo cha ajali hiyo.