Jumatano , 6th Jul , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limethibitisha kumkamata mkazi wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji Peter Moris ambaye ni fundi ujenzi akituhumiwa kwa mauaji ya watu saba wa familia moja katika kijiji cha kiganza mkoani Kigoma yaliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita

Mkuu wa oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamishna Liberatus Sabas

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mkuu wa oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamishna Liberatus Sabas amesema mtuhukiwa Peter Moris amekamatwa mjini kigoma na wamejiridhisha kuwa mtuhumiwa ametekeleza mauaji hayo peke yake kwa kutumia panga na kwamba baada ya kumhoji amedai sababu ni marehemu January Mussa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake.

Aidha Kamishna Sabas amesema wananchi wametoa ushirikiano mkubwa kufanikisha kukamatwa kwake na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ambapo pia ameeleza kuwa idadi ya waliokufa imeongezeka baada ya mtoto aliyejeruhiwa kufariki mkoani morogoro wakati akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya taifa ya muhimbili

Kwa upande wake Mratibu wa kanda ya magharibi wa mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania THRDC Alex Luoga amelaani tukio hilo na kuitaka jamii kutumia njia sahihi na za kisheria kumaliza matatizo.