Alhamisi , 26th Mei , 2022

Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumuua Pankras Petro (62) mkazi wa Nyabishenge, wilayani Kyerwa, baada ya mdogo wa marehemu aitwaye Dominick Petro kuwakodisha watu watatu kwa ujira wa shilingi 50,000, ili wamuue kaka yake kutoka na mgogoro wa shamba.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Maketi Msangi

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Maketi Msangi, na kusema kwamba tukio la mauaji hayo lilitokea Mei 20, 2022.

"Walimjeruhi vibaya Pankras kwa kumkata na kitu cheye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, alikimbizwa hospitali ya Mission ya Isingiro na alifariki siku hiyo akipatiwa matibabu, watuhumiwa hao walikimbilia kusikojulikana, tulianza msako na kuwakamata Mei 25 baada ya kupata taarifa za siri," amesema Msangi.