Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema, mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 20, 2021 majira ya saa 1:00 usiku baada ya Polisi kufanya msako mkali katika Kata ya Kiwira na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo.
Matei amesema hadi sasa wanaendelea kumhoji pamoja na uchunguzi wa kitabibu kwa kushirikiana na wataalam wa afya ili kufahamu endapo alitoa mimba au ana matatizo ya kiafya sambamba na kufahamu sababu ya kufanya tukio hilo la kinyama.