Ijumaa , 18th Aug , 2017

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghirwa ameshindwa kujizua na kumwaga chozi hadharani, alipokuwa akitoa hotuba yake kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akiwapokea watoto Sadia, Doreen na Wilson.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira

Akisoma hotuba hiyo Anna Mghirwa aliwataka watoto hao kuwa mashuhuda wa matendo makuu ya Mungu, na kuwa fundisho kwa madaktari na manesi kwenye utendaji wao wa kazi, na kuwaonya kuhusu vitendo vya kuhujumu, kwani vinachangia kwa kiasi kikubwa upatikananji wa huduma duni za afya.

"Kwa watoto wetu Sadia, Wilson na Doreen naomba niseme kuwa Mungu anawapenda sana, ikawe heri maishani mwenu, na mkawe mashuhuda wa mapenzi na baraka za Mungu kwa wanadamu, ninasema kwa kulia na uchungu kama mama , na kama mzazi ninatambua, ninaomba watoto hawa wakawe ushuhuda kwa manesi na madaktari wetu wanaoiba dawa, wanaoiba dawa, wanalazimisha wagonjwa kununua huduma, inatia uchungu, inauma, ninaomba sana watotoi hawa wakawe alama ya utu, na uadilifu na uzalendo", alisikika mama Anna Mghirwa akisema kwa uchungu.

Leo watoto watatu Doreen, Sadia na Wilson wa shule ya Lucky Vicent ambao walinusurika katika ajali ya gari iliouwa wenzao 32, wamewasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa kitaifa akiwemo Mkuu wa mkoa wa Kilimanrao, Bi. Anna Mghwira.