Jumapili , 23rd Apr , 2017

Ili kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani, Serikali imewataka madereva wa pikipiki kuhakikisha wanapata mafunzo kutoka Veta, huku ikiwaonya wamiliki wa usafiri huo kutowakabidhi madereva ambao hawajapata mafunzo.

Madereva bodaboda

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Seif Shekalaghe wakati akifunga mafunzo ya usalama barabara yaliyoandaliwa na serikali ya wilaya hiyo kwa waendesha pikipiki za kubeba abiria (bodaboda) amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua ama kuisha kabisa.

Ameongeza kuwa wamiliki wa bodaboda wanapaswa kutambua kuwa hiyo ni fursa kiuchumi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanawakabidhi pikipiki watu wenye ujuzi ambao watazilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na ajali zisizo za lazima.

“Wamiliki wa bodaboda mnawekeza fedha nyingi katika kununua bodaboda lakini wengi wenu mnawakabidhi madereva ambao hawana mafunzo na wanakuwa chanzo cha ajali za barabarani. Hakikisheni wamepewa mafunzo na ambao hawana wasaideni wapate ili kuepuka kupoteza pikipiki zenu na nguvu kazi ya taifa kwa ajali ambazo siyo za lazima"- alisema Dk Seif Shekalaghe.