Ijumaa , 5th Feb , 2016

Leo bunge limefanya uchaguzi wa wabunge watakaosimamia taasisi ya bunge pamoja na wabunge ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi washirika wa maendeleo.

Ambao wamechaguliwa katika tume ya utumishi wa bunge ni pamoja na Kangi Lugola, Mussa Zungu, Fakhari Shomari Khamis, Mary Chatanda, Salim Hassan Mtuki na upande wa upinzani utawakilishwa na Magdalena Sakaya pamoja na Mchungaji Peter Msigwa.

Bunge la Afrika litakuwa na uwakilishi wa wabunge wafuatao Mboni Mhita, Asha Abdula Juma, Dkt. Faustine Ndugulile, Steven Masele na upande wa upinzani utawakilishwa na David Silinde.

Jukwaa la wabunge kusini mwa Afrika (SADC) ni pamoja na wafuatao Jamal Kassim Ali, Ester Michael Mmasi, Selemani Jumanne Zedi,Ali Sale Ali, na Magreth Sitta.

Kwa upande wa Bunge la Jumuiya ya madola Tanzania itawakilishwa na Amina Mollel, Maria Kangoye, Zainabu Vulu, Khamis Mtumwa Ali, Salim Rhehani, Jitu Soni, Josephat Kandege, Immaculate, Raphael Chegeni,Juma Omari na Tundu Lissu.

Aidha umoja wa mabunge duniani Tanzania itawakilishwa na Pudensiana Kikwembe, Mohamed Chengella ,Peter Serukamba, Juma Othman na Susan Lyimo.