Jumapili , 20th Sep , 2020

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wawachague viongozi wanaohubiri amani ikiwa ni moja ya tunu ya Taifa hili.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa.

Ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata Bunda Stoo, wilaya ya Bunda, mkoani Mara kwenye mkutano uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Miembeni. . Ambapo Mheshimiwa Majaliwa amesema ni muhimu kwa wananchi kuchagua chama ambacho kitalinda amani ya nchi hii. 

 Amesema uongozi ni lazima utengeneze timu inayofahamiana na inayozungumza lugha moja. “Chama cha Mapinduzi kimeleta viongozi watatu safi. Kwa hiyo ukienda kupiga kura chagua hao watatu ambao ni mgombea urais, ubunge na udiwani.”

 “CCM inaleta tochi inayowaka na kumulika maeneo ya kuleta maendeleo. Ili iwake na kuleta hayo maendeleo, naomba usichanganye betri kwa kuweka gunzi hapo katikati. Je, ukiweka gunzi, hiyo tochi itawaka na kumulikia maendeleo", alihoji Majaliwa.