Onyo hilo limetolewa baada ya siku kadhaa za luteka za kijeshi karibu na kisiwa hicho zilizochochewa na ziara ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi.
Ofisi ya China inayohusika na masuala ya Taiwan imetoa leo waraka unaoeleza jinsi inavyodhamiria kukinyakua kisiwa hicho kupitia shinikizo la kijeshi
Waraka huo umesema China iko tayari kutengeneza nafasi kubwa ya kuungana upya, lakini haitaacha nafasi ya vitendo vya kujitenga kwa njia yoyote ile
China mara ya mwisho ilitoa waraka wa aina hiyo kuhusu Taiwan mwaka wa 2000. Taarifa za hivi punde zimearifu kuwa China imetangaza kumalizika kwa mazoezi yake ya kijeshi kuizunguka Taiwan