Jumamosi , 21st Jan , 2017

Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustino Mahiga amesema China imekubali kutoa fursa za masomo nchini mwao kwa vijana wa Tanzania ambao ndiyo watapewa kipaombele cha ajira katika viwanda vitakavyowekezwa na nchi hiyo hapa nchini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na yanatarajiwa kumalizika kesho tarehe 22 Januari 2017.

 

Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaofahamika kama 'Jogoo', Balozi Mahiga amesema ni wakati sasa kwa watanzania kuchangamkia fursa hiyo ya masomo ili kupata ajira nyingi za watanzania.

Kwa upande wake waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akizungumza katika sherehe hizo Charles Mwijage amesema kuna miradi mingi ya uwekezaji ya China ambayo itawekezwa hapa nchini ikiwemo bandari na viwanda vitakavyoshughulika na teknolojia mbalimbali

Itazame hapa