Jumanne , 28th Mar , 2017

Serikali imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 huku ikionyesha ukomo wa bajeti kufikia shilingi trilioni 31.6 kutoka trilioni 29 za mwaka wa fedha unaoisha Juni 30, mwaka huu

Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango

Katika bajeti hiyo, fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka trilioni 11.8 mwaka 2016/17 hadi trilioni 11.9 mwaka 2017/18 sawa asilimia 38 ya bajeti yote.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa hii leo bungeni mjini Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Akiwasilisha mapendekezo hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ametaja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa ni ujenzi wa reli ya kati, kuhuisha shirika la ndege Tanzania na shamba la kilimo na uzalishaji sukari la Mkulazi.

Aidha, Waziri Dkt. Mpango ametaja changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017 hadi Februari mwaka huu kuwa ni mwamko mdogo wa kulipa kodi na hususani kuzingatia matumizi ya mashine ya kielektroniki.

Baadhi ya wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi, nje ya ukumbi wa bunge wamesema serikali imechukua jitihada kubwa katika kuhakikisha inaondokana na utegemezi kuliko kutegemea fedha kutoka nje.

Wabunge bado wanaendelea na vikao na shughuli za utekelezaji katika kamati mbalimbali hadi Aprili 2 mwaka huu kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April 4 mwaka huu mjini Dodoma.

Huyu hapa Dkt. Mpango pamoja na baadhi ya wabunge ambao ni 

 Zito Kabwe Mbunge wa Kigoma mjini

Japhet Asunga Mbunge wa Vwawa

 Rashid Shangazi Mbunge wa Mlalo