Jumanne , 21st Mar , 2017

Takwimu zinaonesha kati ya wafungwa 4,815 walionufaika na mpango wa Parole (Wafungwa kupewa vifungo vya nje) ni wafungwa 25 pekee ambao walikiuka masharti

Waziri wa Mambo ya Ndani - Mwigulu Nchemba

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Parole na kusema mpango huo una lengo la kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kuisaidia idara ya mahakama kusikiliza kesi za watuhumiwa kwa uharaka.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Parole Mhe. Augustine Mrema amesema kazi yake kwa sasa ni kuhamasisha wananchi waache kufanya vitendo vya kihalifu.

Wakati huohuo waziri Mwigulu amezungumzia suala la haki ya mtuhumiwa hususani anapokamatwa au kushikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano,ambapo amesema jeshi la polisi lina wajibu wa kumuachia huru mtuhumiwa yoyote ambaye anabainika kutohusika katika tuhuma alizoshukiwa.

“Mwenye Makosa ni vizuri kufika kwenye mikono ya sheria, lakini mkijiridhisha kwamba hana makosa, au siyo yeye mliokuwa mnamtafuta, isiwe tabu kumuachia”  Amesema Nchemba

Mtazame hapa