Ijumaa , 4th Dec , 2020

Mkurugenzi wa shirika la  Child Support Tanzania, Noela Msuya, amesema kuwa tatizo la wanafunzi kutoelewa somo la Hisabati ni ulemavu uliojificha.

Hisabati

Ameyasema hayo jijini Mbeya, wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani, na kusema kuwa suala la kutoelewa somo la hisabati nalo ni ulemavu uliojificha na kwamba jambo hilo linahitaji walimu wawe makini na wafahamu wanafunzi wao wanahitaji kitu gani ili waelewe.

"Mfano mimi wakati ninasoma shule ya msingi mwalimu alitupa swali la 25 + 25, mimi niliweka jibu 410 kwa maana nilijumlisha hizo tano nikapata jibu 10, halafu nikajumlisha hizo mbili nikapata 4, kwahiyo jumla ikawa 410, na nikajiona nipo sawa na mwalimu wangu alinimbia nimekosea bila kunisaidia vizuri", amesema Noela.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo yaliyofanyika jana Novemba 3, 2020, ni "Sio kila ulemavu unaonekana".