Jumatano , 19th Jul , 2017

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini, Upendo Msuya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Mtoto wa Marehemu Kelvin Msuya amethibitisha taarifa za msiba na kusema kuwa shughuli za Mazishi zinafanyika Tegeta.

Marehemu Msuya amefariki ikiwa ni miezi miwili baada ya kujiuzulu nafasi yake kama Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania