Jumatano , 18th Jan , 2017

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma ameahidi kumaliza kero ya ucheleweshwaji wa kesi kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika usajili na uendeshwaji wa kesi hizo.

Rais Magufuli akimuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Ikulu Dar es Salaam

Prof. Juma ametoa kauli hiyo mara baada ya kuapishwa na Rais Magufuli kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania katika  hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama ya Kuu na Viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Jaji Prof. Ibrahim Juma amesema atakachoanza nacho ni kupitia sera mpya ya TEHAMA ili kuangalia jinsi ambavyo anaweza kuitumia katika kuiendesha mahakama kisasa zaidi zaidi.

Rais Magufuli katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya rufaa

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma amechukua nafasi ya Mhe.Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma alikuwa Jajiwa Mahakama ya Rufaa.

Rais Magufuli na baadhi ya watendaji wa mahakama