Alhamisi , 17th Mar , 2016

Kesi ya uchaguzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyo mtangaza mbunge wa Njombe kusini Edward Mwalongo inaanza kusikilizwa Machi 18 mwaka huu baada ya kupita hatua ya mapingamizi huku mashahidi wakijulikana siku hiyo.

Aliyekuwa mgombe wa Chadema jimbo la Njombe, Emmanuel Masonga,

Kesi hiyo namba 6/2015 katika mahakama kuu kanda ya Iringa iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombe wa Chadema jimbo la Njombe Emmanuel Masonga ambapo anawashitaki Mbunge Mwalongo, msimamizi wa uchaguzi mkurugenzi wa mji Njombe Eluminata Mwenda na manasheria wa serikali jana ilikuja kwaajili ya kupeleka mashahidi kwa upande walalamikaji.

Akizungumza mahakamani hapo mbele ya jaji Jacob Mwambegele wakili wa Masonga, Edwin Swale amesema kuwa mashahidi wao wameshawaandaa kama mahakama ilivyo wataka kuwasilisha mashahidi ndani ya siku saba.

Jaji Mwambegele amesema kuwa tayari ushahidi huo wameupokea na kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa maandalizi ya awali Machi 18 mwaka huu na kuwataka mawakili wa pande zote mbili kukaa pamoja ili kuangalia vitu vinavyoleta utata vinachunguzwa na kuviweka sawa ili itakapo anza isichukue mda mrefu.

Akizungumza na wananchi waliofika mahakamani hapo nje ya ukumbi wa mahakama Wakili Swale amesema kuwa kesi hiyo inaanza kusikilizwa kwa hatua ya maandalizi.