Jumamosi , 1st Aug , 2015

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo nchini CHADEMA, Edward Lowassa leo amerejesha fomu aliyoichukua kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea urais kupita chama hicho.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.

Akizungumza mara baada ya kukabidhwa fomu Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Prof.. Abdallah Safari amesema mh. Lowassa amemaliza minong'ono iliyokua ikisemwa kwamba huenda asingerudi tena

Katika hatua nyinngine Wagombea wa urais kupitia vyama vya siasa vya Tanzania Labour Party TLP, na UPDP, leo wamejitokeza ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu tayari kwa maandalizi ya kugombea nafasi ya urais kupitia vyama vyao.

Kwa upande wa chama cha TLP mgombea wake wa Urais alikuwa ni Maximilan Lyimo, ambapo chama cha UPDP mgombea wake alikuwa ni Fahami Dovutwa ambapo akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Mgombea wa chama cha TLP Bw. Macmilan Lyimo amehimiza amani kwa watanzania kutokana na uchaguzi wa mwaka huu kuwa na mvuto wa aina yake.

Amesema ni vyama wananchi wakaendelea kuilinda amani ya nchi kwa kuwa uchaguzi ni suala la kupita tu Rais wa nchi anamjua Mungu hivyo hakuna sababu ya watanzanuia wakafarakana na kukosa kuelewana.