Jumanne , 19th Jan , 2016

Aliyekuwa mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa amewapa changamoto mameya wa manispaa ya Kinondoni na Ilala ili kudhihirishia umma kuwa upinzani unaweza kuongoza na kufanya vizuri zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es salaam baada ya kukutana na mameya hao ofisini kwake na kusema manispaa za Jiji la Dar es salaam zimeshindwa kukusanya mapato hivyo kwa kutumia nafasi hiyo wanaweza kuwa vizuri zaidi katika eneo hilo.

Mh. Lowassa ametaka uthubutu wao wa kufanya maamuzi ya busara ambayo yanaonekana kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusimamia ipasavyo shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria zilizowekwa hekima na busara.

Kwa upande wao mameya hao wa Kinondoni na Ilala walisema watafanya kazi kwa kauli mbiu ya mabadiliko na kazi ikiwa ni pamoja na kusimamia ipasavyoshughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi, usafi na ukusanyaji mapato.