Jumanne , 21st Nov , 2017

Kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa NEC, kilichoanza jana Ikulu jijini Dar es salaam kimemalizika leo na kutoka na maadhimio kadhaa ikiwemo uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya mkoa na taifa.

Akitoa maadhimio hayo mbele ya waandishi wa habari leo mchana katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa mwenyekiti wa chama Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wanachama ambao hawajateuliwa kujitathimini na kubaki wanachama waaminifu ndani ya chama.

Polepole pia ametaja majina ya wagombea waliopitishwa na mkutano mkuu kuwania nafasi za Mwenyekiti mkoa, Mjumbe wa NEC, Mwenezi wa mkoa, Mwenyekiti jumuiya ya Wanawake taifa, Mwenyikiti Jumuiya ya wazazi taifa pamoja na Mwenyekiti jumuiya ya vijana taifa UVCCM. Amesema waliokuwa wametuma maombi ya kuteuliwa ni wanachama 3004 kwenye nafasi 261.

Kwa upande mwingine mkutano wa halmashauri kuu ya chama umeacha kupitisha wagombea waliotuma maombi kutoka mkoa wa Magharibi visiwani Zanzibar, baada ya kujiridhisha kuwa wote waliotuma maombi hawakukidhi vigezo.

Aidha mwenyekiti wa chama hicho amewaagiza wanachama walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali kujiepusha na vitendo vya rushwa ili wakachaguliwe kwa haki kwaajili ya kuwatumikia wananchi.

Zaidi tazama video hapo chini.