Alhamisi , 21st Oct , 2021

Mtoto mwenye umri wa siku tatu, jinsia ya kike amekutwa amefariki dunia baada ya kutupwa ndani ya shimo la choo na mwanamke ambaye bado hajafahamika huku Jeshi la Polisi mkoani Mbeya likiendelea na msako mkali kumkamata mwanamke aliyefanya unyama huo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Oktoba 20, 2021, wilayani Rungwe na jeshi hilo limelaani mauaji ya mtoto huyo asiyekuwa na hatia.