Jumatatu , 29th Mei , 2017

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.

IGP (Mpya) Simon Sirro, Kulia ni aliyekuwa IGP Ernest Mangu.

Mangu ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuwa IGP mpya wa kuliongoza jeshi la polisi nchini.

Kuhusiana na hali inayoendelea mkoani ][Pwani, Mangu amesema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano" - Mangu alifunguka

Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.

Sirro ameapishwa leo kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga. Baadaye alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo.