Jumatatu , 1st Aug , 2016

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe, jana ameachiwa kwa dhamana mara baada ya kuhojiwa na jeshi la Polisi kwa takribani masaa matatu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe,

Mhe. Mbowe alihitajika kituoni hapo kuhojiwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi aliyoyatoa wakati wa Mkutano wa waliotangaza Operesheni UKUTA, ambayo imepangwa kuanza September Mosi mwaka huu.

Mhe. Mbowe alijipeleka mwenyewe jana Polisi majira ya Saa saba mchana ambapo aliongozana na viongozi mbalimbali wa Chama hicho akiwemo Mhe.. Edward Lowassa, John Mnyika pamoja na Tundu Lissu pamoja na mawakili wengine wa chama hicho.

Akiongea Mara baada ya mahojiano hayo Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Mhe. Tundu Lissu amesema kuwa Mwenyekiti wao amehojiwa na Polisi kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.

Sauti ya Mbunge Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa CHADEMA