Jumatatu , 27th Feb , 2017

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kunyimwa dhamana na kukaa gerezani kwa zaidi ya miezi mine sasa.

Freeman Mbowe - Mwenyekiti CHADEMA

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe akiwa nje ya mahakama mjini Arusha baada ya mahakama ya rufaa kufuta rufaa za upande wa Jamhuri, amesema kitendo hicho kiliwafanya waichukie mahakama kuona inapewa maelekezo na serikali, kumbe siyo kweli bali ni mchezo mchafu wa ofisi ya DPP.

“Leo mahakama imetufariji sana na kuturudishia imani yetu kwao kuwa ni chombo kilichosimama kwa miguu yake kama Mhimili wake na haipokei maagizo ya serikali” Amesema Mbowe.

 Amesema sakata hilo linawasababisha kupeleka hoja katika bunge lijalo kuwa waangalie wafungwa na mahabusu waliomo ndani, kwani siyo wote waliokaa kwa sababu za kuhusika na makosa, bali wanaonewa.

Aidha amewapongeza majaji kwa kuitaka ofisi ya DPP kushikilia watu kwa misingi ya sheria na badala ya kuitia najisi mhimili huo kwa sababu ya michezo ya kisiasa.