Ijumaa , 9th Apr , 2021

Mbunge wa viti maalum Mh. Conchesta Rwamlaza amesema Watanzania sio wanyonge bali wanauwezo wakipangiwa mipango mizuri na kuelekezwa watasaidia kuleta maendeleo katika nchi.

Mbunge wa viti maalum Mh. Conchesta Rwamlaza

Conchesta amesema hayo leo Jijini Dodoma akiwa anawasilisha maoni yake juu ya mpango wa serikali ambapo amesema binafsi afurahishwi na neno mnyonge.

"Mimi hili neno mnyonge linaniudhi sana, Watanzania sio wanyonge, Watanzania wakipangiwa mipango mizuri, wakaelekezwa wanaweza kufanya kazi yao vizuri na nchi ikapata maendeleo," amesema Mh. Conchesta Rwamlaza.

Aidha, Mh.  Conchesta ameongeza kuwa kuwaita Watanzania wanyonge ni kuwafanya wa ukubali unyonge wao na kuushikilia badala ya kuweka jitihada zaidi katika kuleta maendelo katika taifa lao.