Ijumaa , 4th Dec , 2020

Mbunge wa Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, Deo Ndejembi ameahidi wakulima wa zao la miwa katika jimbo lake kuwaletea wafadhili watakaowekeza zaidi ya Shillingi Bilioni Mbili kwenye kilimo hicho.

Mbunge wa Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, Deo Ndejembi

Ndejembi ametoa ahadi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara jimboni humo, kisha kuwa na kikao kifupi na wakulima wa zao hilo katika Kata ya Dabalo kwa ajili yakusikiliza changamoto zao.

Katika kikao hicho Ndejembi, amewaambia wakulima hao kuwa wapo wafadhili ambao wameonesha nia ya kuwekeza shillingi billioni mbili katika kilimo cha zao la miwa, ili kufanya kilimo hiko kiwe chenye tija na chenye manufaa huku akiwasihi kuweka ushirika wao katika namna ya kisasa zaidi.

Ikiwa ni ziara ya kwanza kwa mbunge huyo jimboni kwake tangua kuchaguliwa kwake, katika ziara yake hiyo amehusisha wataalamu kutoka TARURA ambao alipita nao katika kila barabara yaenye changamoto nakufikia makubaliano yakuanza kufanya maboresho pamoja na ujenzi wa miundo mbinu ilikutatua keroza wananchi.