Ijumaa , 8th Apr , 2016

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kwa Mkoa wa Singida Christina Mughwai amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Aghakan Jijini Dar es Salaam.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kwa Mkoa wa Singida Christina Mughwai

Kwa Mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA,Zanzibar,Salum Mwalimu amesema Mughwai amefariki dunia jana alasiri kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu.

Mwalimu amesema kuwa wamepokea taarifa ya kifo hicho kwa mshtuko mkubwa kutokana na Christina kuendelea kuhitajika katika kulitumikia taifa,chama na wana Singida kwa Ujumla.

Amesema Chama kinawasiliana na familia ya marehemu kujua taratibu za mazishi na mahali ambako atapumzishwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa mbunge katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2010 hadi 2015