Jumamosi , 13th Aug , 2022

Mchungaji wa Kanisa la KKKT Makedonia ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga Dayosisi ya Kusini Mashariki ya ziwa Victoria (Jina limehifadhiwa) anashikiliwa kwa tuhuma za kumlawiti kijana wa miaka nane

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekatwa  August 12 baada ya  Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kupokea malalamiko kutoka mmoja wa familia hiyo

Kamanda Magomi amesema  Jeshi hilo linamshikilia mchungaji wa kanisa hilo ambaye jina lake limehidhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi na taratibu zikikamilika   atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.