Jumanne , 1st Mar , 2016

Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee na Madiwani wawili wa chama hicho jana walihojiwa na polisi kutokana na vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa Meya wa Jiji na kuahirishwa.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee (kulia), akionesha alama ya mbili inayotumiwa na Chadema wakati akisindikizwa na polisi(Picha sio ya tukio la Jana).

Jana mchana Mbunge huyo wa Kawe aliwasili katika kituo kikuu cha Polisi akiongozana na Mbunge wa Bunda Mhe. Esther Bulaya ambapo waliingia katika kituo hicho na kukaa kwa masaa kadhaa na hakukuwa na taarifa kamili ya mahojiano hayo yalihusiana na nini.

Aidha madiwani wawili waliohojiwa na polisi wa kata za Mbezi na Salanga pamoja na Kada mmoja wa Chama hicho ambaye hakuweza kufahamika mara moja nafasi yake ambapo wote walishikiliwa na jeshi hilo kutokana na tuhuma za kuhusishwa na vurugu hizo.

Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa linaendelea kumtafuta Mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Mwita Waitara kwa mahojiano zaidi kutokana n a vurugu hizo.

Uchaguzi wa Meya wa Dar es salaam uliahirishwa siku ya Jumamosi baada ya katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam Therisia Mmbando kutangaza kutofanyika uchaguzi huo kutokana na zuio la Mahakama.