Ijumaa , 24th Oct , 2014

Mifuko ya jamii hapa nchini imeshauriwa kuelekeza nguvu zaidi katika kuwahamasisha wananchi wasio katika sekta rasmi ili kuboresha maisha yao badala ya kuendelea kugombea wanachama walio katika sekta mbalimbali kama ilivyo hivi sasa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi Hawa Ghasia

Rai hiyo imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Hawa Ghasi wakati akifungua mkutano wa Saba wa LAPF jijini Arusha unaowakutanisha wanachama wa mfuko huo waajiri na wadau wengine muhimu wa mfuko huo.

Aidha waziri Ghasia ameiomba LAPF kutazama upya uwezekano wa kuanza kutoa Fao la elimu kwa wategemezi wa wanachama ili kuwapunguzia mzigo mkubwa wanchana wa kusomesha watoto ambao kwa sasa ni changamoto kubwa.

Kwa Upande wake Meneja wa LAPF amesema kuwa mfuko huo utaboresha mafao na kuchangia ya sekta ya elimu ili kueleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla