Jumamosi , 21st Oct , 2017

Mfuko wa udhamini wa Ukimwi nchini Tanzania umekabidhi hundi ya shilingi Milioni 860 za kitanzania kwaajili ya ununuzi wa dawa za zitakazo tolewa kwa wagonjwa wa virusi vya ukimwi wapatao milioni moja na laki nne hapa nchini.

Mfuko huo umeazishwa na serikali kuchangia miradi ya ukimwi kwa fedha za ndani baada ya wahisani kusitisha misaada ya kutoa dawa hizo ambazo ni muhimu kwaajili ya wenye Virusi Vya Ukimwi ambapo kila mwaka Tanzania huitaji dawa zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.8 kuhudumia wenye VVU

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu, Bunge Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kwa pamoja wamesema fedha hizo zitajenga kituo cha afya cha Mererani ili kuwahudumua asilimia 60 ya wachimbaji madini walioathirika na virusi vya ukimwi na kusambaza dawa kote nchini huku jamii ikitakiwa kuchangia kwenye mfuko huo