Alhamisi , 19th Jan , 2017

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli (Kulia) akiwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa walipokutana na kufanya mazungumzo, Ikulu

 

Mhe. Rais Mkapa amesema lengo la kukutanana Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Nimekuja kumu'update' na kumueleza maendeleo ya kazi yangu ya facilitation katika mgogoro wa Burundi kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti, na amenikabidhi kazi ya kusaidia mazungumzo pale ya kupatanisha hawa watu, tulikuwa na mkutano wa siku moja pale Arusha, na pia natarajia nitaripoti kwenye mkutano wa wakuu, mwezi ujao. basi nilikuja kumumpa update" Amesema Mkapa

Waki huo huo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Martin Bille Herman amesema katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.