Ijumaa , 26th Aug , 2016

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema ofisi yake imeanza kutatua hali ya sintofahamu ndani ya baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimeanza kukiuka miiko na utaratibu za usajili wa vyama.

Jaji Mutungi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Baraza la Vyama nchini ambao walikuwa wanajadiliana namna ya kupata muafaka wa kutatua changamoto ambazo zinaendelea kujitokeza ndani ya baadhi ya vyama.

Wakati huohuo Jaji Mutungi amesema ofisi yake imesogeza mbele mkutano wa baraza uliopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 3 na 4 Oktoba.