Jumamosi , 23rd Jul , 2016

Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ubakaji wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Sehemu ya jiji la Mwanza

Taarifa mnamo tarehe 13.07.2016 majira ya saa 10:00 jioni katika mtaa wa Kitangiri kata ya Kitangiri wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, mtuhumiwa Elisha Lameck miaka [18] mkazi wa kitangiri alikutwa akijaribu kumbaka mtoto mdogo (Jina lake linahifadhiwa) mwenye umri miaka 5, nyumbani kwao .

Inadaiwa kuwa siku hiyo mtuhumiwa alifika hapo kwenye hiyo nyumba kuwasalimia na kumkuta msichana wa kazi za ndani aitwaye Zulekha Sameer na mtoto, ndipo alipomchukua mtoto huyo na kuingia naye chumbani kisha akafunga mlango.

Baada ya dakika kadhaa dada wa kazi Zulekha Sameer alishangaa ukimyaa uliokuwepo katika chumba walichoingia ndipo alipokwenda kufungua mlango nakukuta ukiwa umefungwa, ndipo alikwenda dirishani kuchungulia na kumuona mtuhumiwa Elisha Lameck akiwa amevua nguo zote pamoja na mtoto huku akizichezea sehemu za siri za mtoto.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa mfanyakazi (House Boy) wa mama mwenye nyumba aliyejulikana kwa jina la Mama Shakifu ambaye anaishi Uarabuni kwa sasa, na kwasababu aliwahi kufanya kazi katika nyumba hiyo, mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kwenda katika nyumba hiyo kuwasalima.

Mtuhumiwa amekamatwa na yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, huku uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ukiwa bado unaendelea.