Jumatatu , 20th Nov , 2017

Mtoto wa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mke wake Grace, Chatunga Bellarmine Mugabe ameingilia kati kinachoendelea nchini humo kwa kukitukana chama cha ZANU PF huku akisema chama hiko bila Mugabe si chochote.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook Chatunga ameandika ujumbe akiwaambia wanazimbabwe kwamba hawawezi kumfukuza kiongozi wa mapinduzi, na kwamba baba yake atabaki kuwa shujaa wao siku zote.

"Huwezi kumfukuza kiongozi wa mapinduzi, ZANU PF si lolote bila Mugabe, Gushungo atabaki kuwa mshindi wa washindi, najivunia wewe baba, Gushungo ni milele mpaka kifo, watu kama Wellence Mujuru kusherehekea na kuandamana ni kutokana na wivu  na kuigiza kama anajali watu na mashambulio yasiyo ya tija", ameandika Chatunga

Chatunga hakuishia hapo aliendelea kuandika ujumbe mwingine akisema "sote tunakuwa kwenye maisha na kuwa na jukumu la kutumikia nchi yetu, wote tuna jukumu la kuweka nchi yetu salama na kulinda utaifa wetu, Mungu awabariki wale waliojitoa muhanga kwa taifa letu Zimbabwe", huku akimshukuru Rais wa nchi hiyo kwa kuandika kwa lugha ya Kiswahili.

Chama cha ZANU PF ambacho ndio chama kilichoipatia uhuru Zimbabwe kimetaka kiongozi huyo kujiuzulu leo hii,vinginevyo kitachukua hatua dhidi yake.