Jumatano , 11th Jan , 2017

Muft wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry amewataka Masheikh, Maimamu na viongozi wote wa dini ya Kiislamu nchini kuandaa dua maalumu kwa ajili ya kuliombea taifa dhidi ya hatari ya ukame unayolikabili taifa katika msimu huu wa kilimo.

Sheikh Abubakar Zubeiry

 

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza la Waislamu nchini (BAKWATA) Sheikh Khamis Mataka amesema hayo leo kwa niaba ya Mufti Zubeir na kwamba sala hiyo inalenga kutuma toba kwa Mwenyezi Mungu ili aruhusu mvua kunyesha.

Sheikh Mataka amesema taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa zinaonyesha kuwa huenda Tanzania mwaka huu ikakabiliwa na ukame mkali utakaosababisha madhara makubwa kama vile njaa katika maeneo mengi nchini.