Jumanne , 21st Nov , 2017

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu wadhifa wake wa kuiongoza nchi hiyo, jioni ya leo baada ya wabunge kuanza kumchukulia hatua za kumuondoa.

Barua ya kujiuzulu kwake imesomwa  Bungeni ambako wabunge walikuwa wakiendelea na kupiga kura za kutokuwa na imani naye, na kuthibitishwa na gazeti la serikali ya Zimbabwe, 'The Herald'.

Mitaa ya mji wa Harare imeonekana kufurika watu wakifurahia hatua hiyo ya kujiuzulu, huku wakisema hatimaye kachukua hatua za busara.

Robert Mugabe amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1980, huku akiwa na wadhifa wa Waziri Mkuu na kisha kuwa Rais wa nchi hiyo mpaka sasa.