Jumanne , 19th Sep , 2017

Klabu ya soka ya Simba imetua jijini Mwanza alfajiri ya leo Septemba 19 tayari kwa maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC huku Okwi akikabidhiwa mkwanja wake wa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Agust. 

Kwa mujibu wa msemaji wa Simba Haji Manara Simba itaanza mazoezi ya kujiwinda na mchezo wake wa Septemba 21 dhidi ya Mbao FC.

"Timu imewasili leo jijini Mwanza na msafara wote umefika salama, timu itaanza maandalizi ya mchezo wetu wa ligi siku ya Alhamisi", amesema Manara.

Wakati huo mchezaji bora wa ligi kuu mwezi August Emmanuel Okwi, amekabidhiwa zawadi yake ya shilingi milioni moja na wadhamini wa ligi hiyo. Simba ipo katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 7 nyuma ya Mtibwa Sugar yenye alama 9.