Tukio hilo limetokea Septemba 20, 2017 kwenye bomoabomoa ambayo inatekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, yenye lengo la kuandaa eneo ili kupisha mradi mkubwa wa majitaka katika manispaa hiyo.
Wakazi wa eneo hilo wamelalamikia zoezi hilo na kuiomba serikali kuwaonea huruma kwani hawana mahali pengine kwa kwenda kujisitiri.
Pamoja na hayo pia eneo hilo la Jangwani lilishapigwa marufuku kwa wananchi kujengwa makazi, kwani ni eneo hatarishi kutokana na kuwa kwenye mkondo wa mto Msimbazi ambao nyakati za masika hufurika.