Rais Magufuli na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo
Agizo hilo amelitoa hii leo Septemba 20,2020 kwa njia ya simu wakati akiongea na wananchi njiani kuelekea mkoa wa Tabora ambapo amesema fedha hizo ambazo zitatolewa ni kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa barabara ya kilometa kumi kwenda uvinza.
"Mheshimiwa Jafo, niko Uvinza nimeshatoa maagizo TARURA waletee bilioni tano wamalize kilometa zote kumi za kwenda Uvinza, kesho utekeleze na umletee Meneja wa TARURA hizo bilioni tano ashughulikie hii barabara aweke wakandarasi nataka lami wananchi wa'enjoy'", amesema Dkt. Magufuli.
"Zote tengeneza nataka siku nikija hapa jiwe la msingi nataka nije nikute pamewekwa lami hadi uvinza mjini nataka nikalale uvinza", ameongeza.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa anafahamu kwamba Mkoa huo wa Kigoma hasa wilaya uvinza unakabiliwa na tatizo la umeme tangu nchi imepata uhuru ambapo ameahidi kulishughulikia suala hilo.