Jumamosi , 21st Jan , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Januari, 2017 amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anne Kilango

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa inasema kuwa Anne Kilango Malecela ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Huyo anakuwa ni mbunge wa 8 kuteuliwa na Rais Magufuli akiungana na wengine wawili Abdallah Bulembo na Prof. Paramagamba Kabudi walioteuliwa wiki hii.

Pia hii inaweza kuwa ni kuziba nafasi ya Dkt. Abdallah Possi ambaye amejiuzulu ubunge siku ya jana.