Alhamisi , 19th Jan , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi.

Dkt. Possi akiapa mbele ya Rais, baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri mwanzoni mwa mwaka 2016

 

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Dkt. Abdallah Possi itatangazwa baadaye.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah Possi alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.

Kufuatia uteuzi wa Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi, nafasi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu (Ulemavu) itajazwa baadaye.