Jumamosi , 21st Oct , 2017

Shirika la Afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika .

Akifafanua kuhusu uamuzi wa uteuzi huo Mkurugenzi Mkuu mpya wa WHO, Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus, amesifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya kwa umma.

Hata hivyo wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa Rais Mugabe, huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .

Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza shirika la WHO na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.